Rais Kikwete Awaonya Vijana wa CCM Wasiwe 'Makuwadi'

Rais Jakaya Kikwete amewataka vijana wa  CCM kutokuwa makuwadi na madalali wa wagombea urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.
Rais Kikwete aliyasema hayo mjini hapa jana alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu wa CCM.
“Vijana wasigeuke kuwa makuwadi wa kuwahonga vijana wenzao ili wamchague mtu fulani. Kwa kufanya hivyo watakuwa wametoka kabisa nje ya mstari.
“Tunataka vijana watakaosema tunatafuta viongozi wa Taifa hili, ila watu wa aina  hii hapana,” alisema Rais Kikwete.
Alisema lengo la kuanziasha shirikisho hilo ni kuwaandaa vijana hao ili waujue uongozi na waweze kuwa viongozi wazuri katika siku za baadaye.
“Viongozi wa vijana wanasafirishwa wanaletwa hapa Dodoma kwa ajili ya kumsikiliza mzee fulani, ndiyo maana siku hizi hoja ya vijana siyo tishio kwa mtu yeyote kwa sababu hawana mawazo ya kutoa kwa ajili ya kukijenga chama na Taifa,” alisema Rais Kikwete.
Pia, aliwataka vijana hao kuhakikisha CCM  inaendelea kushika dola katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwa hilo ndilo jukumu lao.
“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi tunachotaka sisi ni CCM iendelee kuongoza Tanzania na wapinzani waendelee kuisoma namba kama ilivyokuwa kwa miaka mingine, nawaamini, nina matumaini na nyie pia CC ina matumaini makubwa ya kukivusha chama hiki katika Uchaguzi Mkuu ujao,” alisema Rais Kikwete.

Crdt: Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment