Mrema: Nitalifikisha Gazeti la Jambo Leo Mahakamani

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) na Mbunge wa Jimbo la Vunjo Dr. Augustino Lyatonga Mrema, amekanusha tuhuma za yeye kufukuzwa uanachama wa Tanzania labour party (TLP), kama ilivyo andikwa na gazeti la Jambo Leo na kusema kuwa atalifikisha mahakamani kudai fidia ya kiasi cha Shilingi Billioni mbili kwa kudhalilishwa katika uongozi wake na gazeti hilo, kwa kuandika habari ya upande mmoja ya kumdhalilisha kuwa yeye sio Mbunge na mwanachama wa TLP.

Dr.Augustino Lyatonga Mrema alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya vyombo visivyokuwa na maadili kuandika habari za uchochezi na kumdhalilisha mbele ya wapiga kura wake, na serikali kukaa kimya bila kuchukulia uzito jambo hilo la yeye kufukuzwa uanachama na ubunge Dr. Mrema alitoa wito kwa vyombo vya habari kuacha kumchafua, kwani anamchango mkubwa katika Taifa hili kwani alishawahi kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya ndani hivyo wasitumike vibaya na wanasiasa uchwara ambao hawaja komaa kisiasa, kwani hivi karibuni alikuwa na mazungumzo ya amani na kiongozi Mwadhama Kadinali Pengo ambaye ni kiongozi mkubwa na mwenye kuthamini mchango wake katika Taifa.

Source: Jf
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment