Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi humpata mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuzaa.
Tatizo hili huanza ghafla au taratibu ambapo awali mwanamke alikuwa anapata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mama haelewi au hajielewi jinsi mzunguko wake unavyoenda.
Tunaposema mzunguko unavurugika ni kwamba tarehe maalumu hazieleweki kwa hiyo mwanamke anashindwa kutimiza malengo yake kwa kutumia mzunguko huo. Unaweza kujikuta unapata hedhi ghafla mahali usipotarajia hivyo unabaki na wasiwasi hujui la kufanya kwa kuwa hukujiandaa. Vilevile inaweza kutokea ukapoteza kabisa siku zako, mfano endapo ulitarajia tarehe fulani uingie, mara hakuna dalili na wala huingii.
Malengo katika mzunguko wa hedhi au faida za kuufahamu mzunguko huo ni kwamba; kwanza utakusaidia kuepuka kupata mimba usiyoipangilia, pili utakusaidia kupata mimba uliyoipangilia na tatu utaweza kupanga upate mtoto gani kama ni wa kike au wa kiume.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Kuvurugika kwa mzunguko utagundua endapo utafahamu vizuri mzunguko wako, ili kufahamu mzunguko inabidi ujue siku uliyoanza kuona damu hadi utakapoona tena.Mzunguko daima huwa unatofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.
Tatizo linapotokea linaweza kuwa kwa kurukaruka siku, kupoteza siku yaani mwezi mwingine unaona na mwingine hauoni, au unaingia mara mbili kwa mwezi au unaona damu ya hedhi kwa siku zaidi ya arobaini.Damu ya hedhi inaweza kutokea kidogo kidogo au nyingi huku ikiambatana na mabongemabonge na maumivu. Maumivu wakati wa hedhi husambaa chini ya tumbo hadi miguuni na kiunoni.
CHANZO CHA TATIZO
Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi husababishwa na mabadiliko ya mazingira ambapo mfumo wa mwili pia hubadilika hasa unapotoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.
Matatizo mengine ni hofu, woga, mabadiliko ya kisikolojia, uwepo wa uvimbe kwenye kizazi, matatizo katika mfumo wa homoni, matatizo katika vifuko vya mayai na tabaka la ndani la kizazi pia ni mojawapo ya chanzo cha tatizo hili.
Kuharibika kwa mimba pia huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa ambapo unapata damu bila ya mpangilio na maumivu makali.
Maambukizi sugu ya kizazi pia ni mojawapo ya sababu.
Dalili ya maambukizi sugu ya kizazi ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara ambapo kila ukipimwa unaambiwa ni ugonjwa wa Yutiai kumbe siyo, kutokwa na uchafu ukeni na maumivu wakati wa tendo la ndoa.
UCHUNGUZI NA TIBA
Hufanyika katika kliniki za magonjwa ya akina mama ambapo baada ya vipimo mbalimbali ambavyo daktari ataona vinafaa tiba itafanyika.
Vipimo vya damu, Ultrasound na vingine vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.
Athari za kuvurugika mzunguko ni kutopata ujauzito, maambukizi ya kizazi na kuziba mirija.
Wahi hospitali unapopata mabadiliko katika mzunguko wako wa hedhi.
Crdt: Kandili
Home / Afya
/ Wanawake: Kama Unatatizo la kuvurugika kwa Mzunguko wa Hedhi Kila Mara Bhasi Hili Ndio Tatizo Linakuandama
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment