Sikiliza Alichokisema Diamond Platnumz Kuhusu Kufungua TV yake Hivi Karibuni...




Zarina Hasani aka The Bosslady amesema upendo anaoupata baada ya kuanzisha uhusiano na Diamond Platnumz, umemfanya agundue kuwa watanzania wamemkubali kama mtu wao.

Zari alisema tangu ameanza kuja Tanzania amekuwa akipokea upendo zaidi kutoka kwa watanzania kiasi ambacho kimemfanya ajisikie kama yupo kwao. “Siwezi hata kulalamika, watu wa Tanzania ni wakarimu sana ni watu wazuri sana, kwangu mimi sijapata hata tatizo, siwezi hata kusema kitu chochote kibaya kuhusu watu wa Tanzania,” alisema.

“Wamenikaribisha kama ni mtu wao na sasa mimi ni wao hivyo ni yote ni heri kabisa,” aliongeza. Katika hatua nyingine Zari amesema Tanzania itageuka kuwa makazi yake ya mara kwa mara na mipango iliyopo ni kuanzisha mradi wa kibiashara nchini lakini baada ya kufanya utafiti na kubaini fursa za uhakika.
“Siwezi tu nikafungua biashara hapa eti kwasababu mimi ni maarufu nikafungua tu biashara ya kijinga na nikidhani ninaweza nikauza wazo langu la kijinga kwa watu hapa, wao sio wajinga wanatumia hela zao hivyo nahitaji kubaini wapi kuna hitaji, kipi naweza kufanya na hapo ndipo ntaenda na kuwekeza fedha zangu.”

Lakini hata hivyo kwa upande wake Nasibu Abdul "Diamond Platnumz aliweza kufunguka ya moyoni na kudai kwamba anafikiria kuja na show yao! “Hatutaki kufanya ionekane na sisi tunataka kufanya,”
“Lakini tutafanya kitu ambacho kitakuwa bora ambacho kama tulivyoweza kufanya vitu vingine vikafanyika vizuri hilo nalo likae sawa na kila mmoja alifurahie. Kiwe moja ya vipindi vingine ambavyo watu wanavisubiria wavitazame na kilete maslahi pia
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment