Davido Apost Picha Akiwa na Diamond Studio na Kuandika Ujumbe Uliowacha Midomo Wazi Mashabiki Wake.

 Davido na Diamond Platnumz akiwa studio mwishoni mwa mwaka juzi Tukio hilo lilimfanya Davido aandike mfululizo wa tweets za mafumbo ambazo wengi waliamini kuwa ni madongo kwa Diamond aliyewahi kumshirikisha kwenye remix ya Number One iliyotokea kuwa hit namba moja Afrika miaka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. 

Kambi ya Diamond ilisisitiza kuwa hakuna ugomvi kati ya mastaa hao wawili na hata staa huyo wa ‘Nasema Nawe’ hivi karibuni aliwahi kuupa shavu wimbo mpya Davido kwenye Instagram. 

Lakini vipi kama kweli Davido na Diamond bado ni washkaji? Kwa kile alichokipost Davido kwenye ukurasa wake wa Facebook, huenda wawili hao wakawa wanaendelea kupanga kufanya makubwa baadaye. 

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Davido amepost picha ya zamani akiwa na Diamond kwenye studio yake nchini Nigeria. Kwenye picha hiyo, Davido ameandika: I think I just recorded a sweeter love song than AYE .. Hmm this album yo.”


Picha hiyo imevutia comments nyingi japo asilimia kubwa ni za wakenya wanaomnyeshea mvua ya matusi! Yes, Wakenya hawataki kumsikia tena Davido! Hakuna shaka kuwa staa huyo wa Nigeria ana picha nyingi ambazo angeweka kuambatanisha na ujumbe huo.


 Hivyo, uchaguzi wa picha akiwa na Diamond unaweza ukawa na dhumuni maalum!
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment