Kamanda wa Polisi Akanusha Kuwepo kwa Magaidi

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabasi, amekanusha taarifa zilizoenea leo katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kukamatwa kwa mtu mmoja aliyevalia vazi la baibui akiwa na bomu Mkoani humo na kusema habari hizo siyo za kweli na ni uzushi.
Mapema asubuhi ya leo kumekuwepo na taarifa ziliyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii zikisema kuwa Maafisa wa Usalama Mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo wamekamata gari aina ya Toyota Premio nyeusi ikiwa na watu wanne huku wakiwa na bunduki nne aina ya SMG na risasi 160 wakijaribu kuingia Chuo cha Uhasibu Arusha-IAA.
Hata hivyo taarifa za kiusalama kutoka IAA zinasema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba wananchi wazipuuzie.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment