Diamond Platnumz Apewa Fidia ya Milioni 14 za Ujenzi wa Ukuta wa Nyumba yake Iliyoporomoka na Mafuriko


 Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amekabidhiwa hundi ya zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya kufidia ujenzi wa upande wa nyumba yake uliodondoka.
Wakati akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Kampuni ya Bima ya UAP kwa ushirikiano na Benki ya CRDB, Diamond alisema ukuta wa nyumba yake ulianguka wakati akiwa anamuuguza mama yake aliyekuwa katika hali mbaya.
“Ilikuwa ghafla ukuta wa nyumba yangu ya Tegeta ukaanguka wakati huo nilikuwa natakiwa kulipia fedha kwa ajili ya kurekodi wimbo wangu mpya.“Hivyo nisingekuwa nimejiunga na bima sijui sasa ningekuwa kwenye hali gani? Ni kipindi kigumu sana kwangu,’’ alieleza Diamond huku akiwataka Watanzania wajiwekee bima kwa kuwa ina msaada mkubwa unapopatwa na majanga mbalimbali ya vitu ulivyokatia bima hiyo.
Naye, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa UAP, Raymond Komanga, aliwasisitizia Watanzania waondoe fikra za kwamba bima inayokatwa ni ya gari pekee bali wakate bima za aina mbalimbali.
Chanzo: Mtanzania
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment