Diwani wa Chama cha Chadema Apewa Adhabu ya Kufua Kuzibua Mitaro ya Maji Machafu Pamoja na Mashuka ya Hospitali

Mahakama ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imempa adhabu ya kufua mashuka ya wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Kakonko  na kuzibua mitaro ya barabarani Diwani wa kata ya Kasanda  kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yeye na wenzake wanne kwa muda wa siku kumi na nne baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu.
Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Kibondo Erick Marley,mwendesha mashitaka wa polisi Peter Makala alimtaja Diwani huyo kuwa ni Dikson Barutwa(40)na Daudi Obadia(32)Hatari Kasase (33)Brighton Jona(29)wote wakazi wa kata ya Kasanda Wilayani Kakonko.
Mwendesha mashtaka alisema kuwa mnamo novemba 8 mwaka jana majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha kaziramihunda watuhumiwa wote kwa pamoja walifika katika ofisi ya Ofisa mtendaji wa kijiji hicho isivyo halali na kuifunga ofisi hiyo kwa kuweka gundi aina ya super gluu na unga wa ngano kwenye kufuli ili kumzuia mtendaji asifanye kazi yake.
Inadaiwa kuwa watu hao walifikia uamuzi huo kwa madai kuwa hawamtaki mtendaji huyo wa kijiji Amos Peter na kumtishia kuwa watamuua.
Kufuatia hali hiyo Diwani huyo na wenzake,Mahakama ya Wilaya ya Kibondo imewahukumu kulipa faini ya shilingi elf 50 au kufungwa jela miezi mitano kwa kosa la kufunga ofisi ya mtendaji,na pia kulipa faini ya shilingi elf 50 au kwenda jela miezi miwili kwa kosa la kufanya fujo.
Watuhumiwa wote walilipa faini na kuachiwa huru isipo kuwa Hatare Kasase(33)ambaye anakabiliwa na kesi nyingine ya mauaji hivo alirudishwa gerezani.
Aidha katika kosa la kutishia kuua Diwani huyo na wenzake watatu wamehukumiwa adhabu ya kazi za kijamii ambayo ni kufua mashuka ya wagonjwa katika hospital ya Wilaya ya Kakonkokwa muda wa wiki moja na kuzibua mitaro ya barabara kwa muda wa wiki moja pia.
Ambapo tayari wameshakabidhiwa katika idara ya maendeleo ya jamii kwaajili ya kuanza adhabu hiyo.
Watuhumiwa wengine kayika kesi hiyo waliachiwa huru baada ya kukutwa hawana hatia, waliochiwa huru ni Bonifasi Obadia(35)Amos buseni(33)majaliwa Charles(24)pamoja na Samora Barichako(35)wote wakazi wa kijiji cha kaziramihunda
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment