Mgomo wa madereva wa mabasi ya kwenda mikoani na daladala jijini Dar es Salaam umesababisha maisha ya wakazi wa jiji hilo kuwa magumu, huku mabomu ya machozi yakirindima katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya kwenda mikoani.
Hali ni tete, abiria wanatembea, hakuna safari wa daladala wala mabasi ya kwenda mikoani.
Leo asubuhi Aprili 10, 2015 mtandao wa habari5.com umetembelea maeneo ya Kariakoo, Ilala, Buguruni, Gongo la Mboto, Mbagala, Temeke, Kimara, Ubungo, Sinza, Tangi Bovu hadi Tegeta na kushudia mamia ya abiria wakiwa kituoni wakisubiri usafiri kwa kwenda katikati ya Jiji la Dar es salaam.
Daladala zilizojaribu kubeba abiria katika kituo cha Gongalamboto limevunjwa vioo na watu wanaosadikiwa kwamba wanapinga mgomo huo, huku wengine waliokuwa wakizua mabasi ya kwenda mikoani wakifyatuliwa mabomu ya machozi katika Kituo cha Ubungo.
Katika eneo la Bamaga na Ubungu mamia ya watu wameonekana asubuhi ya leo wakitembea kuelekea Kariakoo na wengene maeneo ya Posta ambao wanafanyia shughuli zao.
Mwandishi wa habari hizi ameshudia polisi wakiwa wametanda katika eneo la Ubungo wakiwa na magari ya maji ya kuwasha na gari ambazo zimebeba polisi.
Katika kituo cha mabibo hakuna daladala lolote kwa ajili ya kuelekea Karikooo wala Mwananyamala.
Pia, leo matrafiki ni wachache sana. Kuanzia Tegeta kupitia Bamaga, Sinza Madukani, Shekilango hadi Ubungo wameonekana matrafiki wawili jambo ambalo si kawaida. Siku za kawaida matrafiki kupitia njia wanakua zaidi 14.
Kutokana na hali na endapo hali itaendelea kuwa kama ilivyo asubuhii, ina maana usafiri wa kurejea majumbani utakuwa mgumu sana na inawezekana abiria wanaokaa mbali Tegeta, Boko, Mbagala, Gonga la Mboto, Pugu, Kiluvya na Kibaha wanakabiliwa na wakati mgumu kwani watalazimika kutumia fedha nyingi kufika nyumbani tena usiku mkubwa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment