Naibu Spika wa Bunge Azirai Ghafla Baada ya Kushambuliwa kwa Hoja

Naibu spika wa Bunge la Kaunti ya Kisumu Bi Pamela Omino alizirai na kukimbizwa hospitalini baada  ya kuvutana na wawakilishi wa kaunti hiyo.
Mzozo huo ulianza  muda wa saa nane mchana baada ya Bi Omino kumzuia Kaimu Spika Gabriel Ochieng na mbeba rungu la bunge kuingia katika bunge hilo.
Bi Omino alisema kuwa yeye ndiye spika halali wa nafasi hiyo lakini wabunge wa hawakuafikiana naye na walisema kuwa nafasi hiyo ni ya Bw Ochieng aliyechaguliwa kama kaimu.
Hata hivyo mama huo alishikilia msimamo wake na kuibua mvutano baina yake na wabunge ambao walimshtumu kwa kuhujumu shughuli za bunge.
Mambo yalibadilika baadaye baada ya wabunge hao kulazimisha rungu liingizwe bungeni ambapo Bi Omino alifuata nyuma lakini alizuiliwa na walinzi wa bunge kabla ya mvutano mkubwa kutokea.
Katika hali hiyo, Bi Omino alizirai na kuibua mvutano mwingine kati ya wabunge hao kabla ya wasaidizi wake kulazimika kumpeleka hospitalini.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment