Polisi Washindwa Kumhoji Gwajima

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, jana lilishindwa kuendelea kumhoji Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuhusu tuhuma za kumtukana Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jana asubuhi,ikiwa ni siku mbili tangu aliporuhusiwa kutoka katika Hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Wakili wa askofu huyo, John Mallya alisema jana kuwa mteja wake alifika kituoni hapo saa 2.10 asubuhi, lakini Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Dar es Salaam alipomuona, alisema hawawezi kumhojiano kwa kuwa afya yake haijaimarika.
“Alitutaka turudi na badala yake kufike kituoni hapo Aprili 9, mwaka huu,” alisema Wakili Mallya aliyeongozana na Askofu Gwajima pamoja na wachungaji wanane wa kanisa hilo.
Askofu Gwajima alijisalimisha mwenyewe  kituoni hapo Ijumaa iliyopita, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Jeshi la Polisi, akituhumiwa kumkashfu Kardinali Pengo wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Dar es Salaam, wakati akiendesha ibada kanisani kwake.
Awali, wakati akihojiwa, aliishiwa nguvu na hatimaye kupoteza fahamu, hivyo kupelekwa hospitali kwa matibabu.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema Askofu Gwajima lazima atahojiwa na ofisi yake ili kujiridhisha zaidi na shughuli anazozifanya, ikiwamo umiliki na uhalali wa kutumia eneo la Kiwanja cha Tanganyika Packers, kilichopo Kawe.
Makonda aliyezungumza kauli hiyo akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani hapo, alisema lengo la uamuzi huo ni kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Credit: Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment