Mwigulu Nchemba Afurahia Kufananishwa na Sokoine

Naibu waziri wa fedha na mbunge wa jimbo la Iramba , Mwigulu Lameck Nchemba amesema anafurahishwa na yeye kufananishwa na aliyekua waziri mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine na kusema hicho ni kitu kizuri kwake.

“Mwenzangu a alikua waziri mkuu najua mimi sio waziri mkuu lakini kufananishwa nae basin i ishara tosha ya kuwa name ni kiongozi bora,labda ni njia ya mimi kuwa kama hivyo”, alisema Nchemba.

Pia Nchemba alielezea juu ya taasisi mbalimbali zinazofanya utafiti juu ya viongozi nchini ambapo amesema tafiti zitolewazo ni kipimo tosha kwa kazi yako.

Nchemba amekua kwenye matokeo mazuri kwenye tafiti mbalimbali zifanywazo na taasisi kuhusu uwajibikaji na ukubalikaji wa viongozi kwa jamii. Nchemba amesema anafurahishwa na tafiti hizo kwani wanaona mabadiliko juu ya utendaji kazi kwa mazoea na wanaona mgawanyo sawa wa matunda ya taifa kwa kila mtanzania.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment