Tazama Picha: Diamond Amvisha Pete ya Uchumba Zari


Mambo yanakwenda kasi, Maisha yanabadilika, Kama kwako maisha yanakwenda mwendo wa kinyonga basi una bahati mbaya, lakini kwa Zari mambo yanakwenda kasi ya ajabu. Zari amevishwa pete na Diamond Platnumz. Wengi wanajiuliza kuhusu pete hiyo.
Watu wa karibu na Zari ambao ni Watanzania walianza kuweka picha mitandaoni inayoonyesha kiganja cha mkono ambacho kinafanana na cha Zari na wapambe wa mwanadada huyo wakatoa siri kwamba shughuli ya kuvishwa pete ingefanyika siku mbili baadaye tangu walipoweka picha ya kiganya kwenye mitandao.



Siku ilipofika marafiki/wapambe hao wakatambulisha rasmi kuhusu ishu hiyo ya pete ya uchumba na hali ya ujauzito ya mwanadada huyokutoka Uganda.

“Siku ya ukumbusho wa kuzaliwa kwa Aunty Ezekiel, nilikutana na Diamond ambaye alionekana kuzidiwa kichaa cha mapenzi, nilimpa moyo na kumweleza kuwa angesubiri ili apate afueni aendelee mbele na angekuja kutulia. Nilimwambia matatizo hayampati mtu asiyekuwa na jawabu na ukiona una matatizo na huna jawabu ujue umefeli na sasa amempata nwanamke ambaye ni mchumba kwa sasa na ameshamvalisha pete,” anasema le mutuz.

“Ukikutana na mpenzi mpya utakuwa kichaa kutaka kujua mambo yake ya zamani ili yakusaidie nini? Baba yangu aliniambia mwanamke ni kisima labda umemuona mtu anachota maji, lakini akija mwingine hawezi kujua kama kilichotwa. Mapenzi si mchezo naona kuna watu wanayazungumzia kama mchezo wa Yanga na Simba na binadamu unaheshimika kwa misimamo.

Diamond hajazungumzia kuhusu pete hiyo wala Zari.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment