Chama cha ACT wazalendo kimeitaka serikali kutoa taarifa ya tume ya uchunguzi wa ajali za barabarani zilizofanyiwa utafiti ili kuweza kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na ulemavu kwa wananchi.
Wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Singida na viunga vyake kwenye mkutano wa kunadi chama cha ACT Zitto Kabwe ,amesema aliyekuwa waziri wa uchukuzi Dk Harsson Mwakyembe aliunda tume ya uchunguzi wa ajali na mpaka sasa majibu hayaja tolewa,jambo ambalo limekuwa likisababisha ajali kuendelea kutokea na kwa kipindi cha mwenzi Machi na April mwaka huu zaidi wa watu mia nane wamepoteza maisha kwa ajali.
Pia Zitto Kabwe ameitaka serikali kuhakikisha inawabana wamiliki wa mabasi kote nchini watoe mikataba ya kazi kwa madereva wao ili waweze kujulikana kwa kufanya hivyo ajali zitapungua.
Awali mwenyekiti wa chama hicho Bi.Anna Mghwira na kada wa chama hicho Bwana Selemani Msindi maarufu kwa jina la Afande Sele wamesema huduma nyingi hasa za afya wakati wa zamani zilikuwa zikipatikana kulingana na uwezo wa serikali wakati ule na kwasasa nchi imekuwa na utajiri mwingi wa madini ,kilimo na biashara, lakini cha kushangaza fursa hizo zimekuwa zikitumiwa na baadhi ya watu wachache na kuwaacha wananchi wengi wakiwa masikini.
0 comments:
Post a Comment