Mtanzania aliyekamatwa Kenya akidaiwa kuhusika na tukio la ugaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa lililosababisha vifo vya watu 150, Rashid Charles Mberesero (20) alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Bihawana, lakini uongozi wa shule alipokuwa anasoma umesema alitoweka shuleni hapo tangu mwezi Desemba mwaka jana.
Habari zilizothibitishwa na wazazi wake ni kuwa mwanafunzi huyo anasoma katika Shule ya Sekondari ya Bihawana Dodoma mara baada ya kufaulu katika Shule ya Sekondari Gonja mkoani Kilimanjaro.
Habari zilizothibitishwa na wazazi wake ni kuwa mwanafunzi huyo anasoma katika Shule ya Sekondari ya Bihawana Dodoma mara baada ya kufaulu katika Shule ya Sekondari Gonja mkoani Kilimanjaro.
Taarifa hizo zimekuja wakati Mberesero maarufu kwa jina la Rehani Dida, akitarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Nairobi baada ya watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani juzi.
0 comments:
Post a Comment