Mgogoro ACT Tanzania Waendelea kufukuta Kwa Kugombea Madaraka ya Uongozi

Mgogoro wa kimajukumu umeanza kuibuka ndani ya chama kipya cha ACT-Wazalendo ambapo mwenyekiti wa taifa wa chama hicho bi Anastazia Mghwira jana alitishia kuachia ngazi.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya chama hicho zinadai kuwa kiongozi mkuu wa chama Kabwe @ Zitto alimuonya mwenyekiti huyo kuwa anaingilia majukumu ya kukieneza chama ambayo kimsingi si yake.

Kwa mujibu wa katiba ya ACT-Wazalendo, kazi ya kukieneza chama ni ya kiongozi mkuu ambapo mwenyekiti kazi yake ni kuongoza vikao vya chama na kusimamia maadili ya wanachama.

Kufuatia mgogoro huo mwenyekiti huyo alitishia kujiondoa ndani ya uongozi wa chama hicho kutokana na mkanganyiko wa kimajukumu kati ya mwenyekiti na kiongozi mkuu. 


Crdt: JF
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment