Hussein Machozi Kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu Ujao.

Star wa bongo flava anayeiwakilisha kanda ya ziwa, Hussein Machozi yuko kwenye mazoezi makali ya kujiweka sawa kwa ajili ya kukipiga na moja kati ya timu inayoshiriki ligi kuu bara msimu ujao.

Akizungumza kupitia kipindi cha “Hatua tatu” cha Times fm, Hussein amedai msimu ujao atasakata gozi kwenye ligi kuu bara na timu ya Kagera sugar.

“Nipo mazoezini sasa hivi kwa ajili ya kujiandaa na kusajiliwa na Kagera Sugar kwa ajili ya kuichezea msimu ujao, so mazoezi wanakuja wananitazama kila siku, kwa hiyo mashabiki watambue msimu ujao wataniona kupitia soka” alisanua Machozi.

Katika line nyingine amesema ilikuwa aichezee muda mrefu Kagera Sugar, lakini hakukuwa na maelewano mazuri kati yake na kocha wa walima miwa hao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment