Breaking News: Basi la Unique Lapata Ajali Lagongana na Lori na Kusababisha Vifo vya Watu 10 na Majeruhi 51

Habari tulizozipata hivi punde kutoka shinyanga zinataarifu kuwa  jeshi la Polisi wakisaidiana na raia wanaendelea kuokoa majeruhi na maiti wa ajali ya gari iliyotokea muda wa masaa mawili yaliyopita kwa kuuhusisha basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora kugongana na lori katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, RTO Chacha Marwa amebainisha kuwa, hadi sasa ni watu 10  ndiyo waliopoteza maisha huku watu 51wakijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitalini.
Tarifa kamili pamoja na picha za tukio ya ajali zitakujia hivi punde usicheze mbali na Sbm broadcast au sikiliza moja kwa moja sbm radio kupitia Sbm radio kupata updated ya tukio zima 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment