Tanzania Yajipanga Kupambana na Mashambulizi ya Ugaidi

Waziri wa Mambo ya ndani nchini Tanzania amesema nchi yake ipo katika tahadhari kufuatia taarifa za vyombo vya habari nchini kwamba, kuna uwezekano wa shambilio la ugaidi katika miji ya Dar es salaam na Mwanza.

Alisema hayo baada ya taarifa kuripotiwa kwamba mmoja wa watu waliokamatwa katika shambulio la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya ni Mtanzania.

Waziri wa mambo ya ndani , Matthais Chikawe, aliiambia BBC,mpaka sasa Serikali ya Tanzania haijaweza kudhibitisha ripoti zinzaoenea ,kuhusu shambulio la ugaidi nchini humo.

Hata hivyo amesema vyombo vya dola nchi nzima viko macho na vimejitayarisha kwa lolote.

Pamoja na hayo waziri Chikawe amesema kuwa serikali ya Tanzania, inafahamu kuwa mmoja ya watuhumiwa walikokamatwa huko Garissa Kenya ni Mtanzania.

Hata hivyo amesema watawasiliana na polisi wa Kenya wakimaliza kumhoji mtuhumiwa huyo.

Tanzania ilikumbwa na shambulio la ugaidi mwaka 1998 wakati mabomu yalilipuka katika balozi za Marekani, jijini Dar es salaam na Nairobi, Kenya na kusabibisha vifo ya watu wengi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment