Kafulila: Nina Marafiki CCM, Chadema Mbona Sihusishwi Kuhamia huko?

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, amekanusha kuhamia chama cha kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania).

Kafulula alisema kuwa hana sababu ya kuhama chama hicho na kukiri kuona katika mitandao ya kujamii habari kuwa anahama chama chake na kuhamia ACT jambo ambalo halina ukweli wowote.

Aloiendelea kusema kuwa huenda tetesi hizo zimekuja baada ya kuwa na marafiki wengi wa chama hicho na kusema kuwa urafiki na wanachama hao hauna maana kuwa anahamia chama hicho.

Hata hivyo Kafulila amehoji ana urafiki na wanachama wa Chadema, CCM, na vyama vingine mbona hawajavitaja, na kudai kuwa Zitto, amehama kutokana na kuwa na migogoro na chama chake lakini yeye hana sababu ya kuweza kukihama chama chake.

Ameongeza kuwa atabaki kuwa Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, na kuendelea na kampeni za kujenga chama hicho ikiwemo yeye kurudi bungeni pamoja na chama hicho kuongeza wabunge wengi zaidi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment