Video: Mourinho Kujadili Kisago Cha PSG

Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameahidi kukutana na wachezaji wake hii leo na kuzungumzia kinaga ubaga kilichowatupa nje katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa hasara ya bao la ugenini la mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG.
Mourinho, amesema hana budi kufanya hivyo kwa lengo la kuwapa nafasi wachezaji wake kujifikiria kwa kina baada ya mambo kuwaendea kombo usiku wa kuamkia hii leo wakiwa nyumbani Stamford Bridge.
Amesema anajua wachezaji wake wanafahamu kwa kina nini kilichowasibu uwanjani mpaka wakashindwa kufikia lengo la kusonga mbele, kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ili hali wapinzani wao walikua pungufu baada ya Zlatan Ibrahimovic kuonyeshwa kadi nyekundu.
Hata hivyo meneja huyo akagusia jambo la kushindwa kwao katika mchezo huo kwa kusema wazi kwamba PSG walionyesha uwezo mkubwa dhidi yao, hivyo walikua hawana namna ya kufanya zaidi ya kupambana hadi mwisho na kwa bahati mbaya matokeo yamewaumiza.
Wakati huo huo Jose Mourinho amesema atakuwa mwendawazimu kujutia baada ya kushindwa kufikia malengo yake katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya zaidi ya kuheshimu kilichotokea uwanjani hapo jana.
Amesema ni wakati mzuri sana kwake kujipanga kwa ajili ya ushindani wa ligi kuu ya soka nchini England ambapo ana nafasi kubwa ya kukiwezesha kikosi chake kuwa kinara msimu huu.Katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliochezwa majuma mawili yaliyopita huko Parc des Princes jijini Paris, Chelsea walilazimishwa sare ya bao moja kwa moja, na usiku wa kuamkia hii leo walilazimishwa matokeo ya mabao mawili kwa mawili.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment