Dk. Slaa Akabidhi Msaada kwa Waliokumbwa na Maafa Kahama Leo

Wakati wananchi wakitafakari njama za kutaka kumuua Dk Willbrod Slaa, amekwenda Kahama kwa ajili kukabidhi mchango wa Chadema kwa watu waliokumbwa na mvua ya mawe iliyosababisha nyumba kubomoka na kuua watu wengi.

Dk Slaa amelakiwa na wananchi wa Mwakata-Kahama leo waliokubwa na maafa hayo wiki iliyopita.

Kiongozi huyo amewasilisha mchango wa Chadema kwa Kamati ya Maafa. Mchango huo ni mabayi 800 yenye thamani ya Sh 12 milioni.

Dk Slaa aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kwamba chama chao cha Chadema ambachokinaongoza serikali ya kijiji hicho kipo nao bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.

Taarifa zinaeleza kuwa baadae mchana Dk Slaa atakuwa na mkutano wa hadhara katika eneo la Isaka, Jimbo la Msalala.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment