Mshambulaiji wa pembeni kutoka nchini Uingereza Adam Johnson amerejea mazoezini baada ya uongozi wa klabu ya Sunderland kutengua adhabu ya kumsimamisha.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alisimamishwa na uongozi wa klabu ya Sunderland mapema mwezi huu, kufuatia sakata la kesi iliyokua ikimuandama ya kutembea kimapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15.
"Uongozi umejadiliana kwa kina na kuafiki suala la kumrejesha kundi Johnson, kutokana na hali ya sasa inayoendelea kwenye chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England PFA (Professional Footballers' Association) ambacho kiliingilia kati suala hilo." Ilieleza taarifa iliyothibitisha kurejeshwa kwa Adam Johnson
"Katika majadiliano hayo, uongozi umeamua kwamba kuna haja kwa mchezaji huyo kurejea kundini kutokana na PFA kuwasilisha utetezi wake na umeonekana una tija kwa maslahi ya mchezaji pamoja na klabu.
"Hivyo uchunguzi uliokua unafanywa na klabu kutokana na kadhia iliyoibuliwa na Adam Johnson unasitishwa." Iliongeza taarifa ya Sunderland FC.
Kurejea kwa Adam Johnson mazoezini huenda kukamuwezesha meneja mpya wa klabu hiyo Dick Advocaat kuwa na matumaini makubwa ya kumtumia kwenye mikakati ya utendaji wake wa kazi ambao ulianza mara moja baada ya kutangazwa kuwa mrithi wa Gus Poyet siku mbili zilizopita.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment