Uchaguzi mkuu wa Urais pamoja na wabunge unatarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu ambapo joto la kisiasa limeanza kupanda huku vyama vya siasa vikihaha kuhakikisha kwamba wanaingia Ikulu Magogoni jijini Dar es salaam.
Mwaka huu wanawake wamezidi kuhamasika na kuhamasishwa kutangaza nia ya kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea urais nchini Tanzania suala ambalo linaweza kubadilisha historia ya Tanzania kwa kuwa miaka marais wote waliowahi kuongoza nchini Tanzania hakuna Rais Mwanamke.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Morogoro, Rais Kikwete amezidi kuwatia hamasa Wanawake kufuatia kuwataka kujiamini na kutohofia kuwania urais huku akisisitiza kuwa wanawake wanaweza na hawakuwahi kumuangusha.
Ameongeza kwa kuwataka wanawake waache uoga wa vitisho vya aina yeyote kwa kuwa wengi wao wameonesha uwezo mkubwa katika nafasi mbalimbali za uongozi katika kipindi cha awamu yake.
Ushirikishwaji wa wanawake katika uongozi umeifanya Tanzania kuwa mingoni mwa nchi 20 zinazo ongoza dunia na nchi ya tano katika bara la Afrika katika suala la uwezeshaji wa wanawake.Suala linalothibitisha kwamba wanawake wanaweza kuliongoza taifa la Tanzania.
Hadi sasa kuna nchi sita duniani zinazoongozwa na wanawake. Nchi hizo ni Korea Kusini Bi Park Geum-hye, Ellen Johnson Sirleaf rais wa Liberia, Dilma Vana Rousseff ni rais wa Brazil, Cristina Fernández de Kirchner rais wa Argentina, Tarja Kaarina Halonen ni rais wa nchi ya Finland, pamoja na Sheik Hasina Wajed rais wa sasa wa Bangladesh.
Katika hatua nyingine Takwimu zinaonesha kuwa wanawake Mawaziri wapo 16, manaibu 20, Makatibu wakuu 8, Naibu katibu wakuu 19 Majaji 40, Mabalozi 13, Wakuu wa mikoa 11, Makatibu Tawala 13 na wakuu wa wilaya 71.
0 comments:
Post a Comment