Mabingwa Wa Hispania Wachanja Mbuga Ulaya

Mabingwa wa soka nchini Hispania Atletico Madrid wamesonga mbele baada ya kufanya kazi ya ziada mbele ya Bayer 04 Leverkusen kutoka nchini Ujerumani katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya wakati wa mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Ateltico Madrid walifanikiwa kurejesha bao moja walilofungwa nchini Ujerumani majuma matatu yaliyopita, hali ambayo ilipelekea muamuzi kutoka nchini Italia, Nicola Rizzoli kuongeza dakika 30 ambazo hazikuzaa matokeo zaidi.

Kutokana na hali hiyo Nicola Rizzoli aliamuru mikwaju ya penati ipigwe kwenye uwanja wa Vicente Calderón huko mjini Madrid na ndipo wenyeji walipofanikiwa kupata penati tatu dhidi ya mbili za wageni wao kutoka mjini Leverkusen nchini Ujerumani. Meneja wa Atletico Madrid, Diego Pablo Simeone amesema umahiri na ushujaa wa wachezaji wake ulikua chanzo cha kufanikisha mipango waliyokuwa nayo tangu kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulishuhudia wakibamizwa bao moja kwa sifuri.

Simione, amesema wachezaji wake hawakutatishwa tamaa na matokeo hayo na badala yake waliendelea kujiamini na kurejesha matokeo kuwa bao moja kwa moja na ndipo walipokwenda katika uhodari wa kuonyeshana umahiri wa kupigiana penati ambapo amesisitiza siku zote inapifika hatua hiyo huwaamini sana wachezaji wake.

Kwa matiki hiyo sasa Atletico Madrid wanaungana na AS Monaco kwa kujumuika na klabu nyingine zilizotangulia kwenye hatua ya robo fainali kama Real Madrid, FC Porto, PSG na FC Bayern Munich.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment