Lowasa Achangiwa Shilingi Laki 7 na Masheikh Kuchukua Fomu ya Kugombea Urais

 Masheikh zaidi ya 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania urais 2015.

Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu na Alli Mtumwa wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.


walisema kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.

Lowassa aliwaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment