FC Barcelona Wamponza Ronaldo, Kufungiwa Hispania

Mshambuliaji kutoka chini Ureno, Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro yupo hatarini kuadhibiwa na shirikisho la soka nchini Hispania kufuatia kitendo cha kushabikia alichokionyesha mara baada ya kuisawazishia Real Madrid wakati wa mchezo wa ligi ya nchini humo dhidi ya FC Barcelona uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Ronaldo ambaye alisajiliwa na Real Madrid mwaka 2009 akitokea nchini England alipokua akiitumikia klabu ya Manchester United, alionyesha kitendo cha kuwaashiria mashabiki wa FC Barcelona kutulia kama sehemu ya kushangilia bao alilolifunga dakika chache kabla ya mapumziko.

Mwenyekiti wa kamati inayosimamia ligi ya nchini Hispania (LFP) Javier Tebas, ameahidi watakifanyia uchunguzi wa kina kitendo hicho kwa lengo la kujua nini Ronaldo alichokimaanisha.

Tebas, amesema hawapendezwi na vitendo cha wachezaji kuonyesha ishara fulani wanapokua uwanjani, hali ambayo wanahisi huenda ikaleta hatari ama maafa kwa baadhi ya watu kutokana na wanavyoelewa ama kutafsiri vitendo hivyo.

Hata hivyo kiongozi huyo hakusema ni muda gani itawachukua kufanya uchunguzi wa kitendo hicho cha Ronaldo, hivyo huenda wakati wowote wakatangaza maamuzi ya walichokibaini kupitia uchunguzi wanaoufanya.

Katika mchezo huo wa mwishoni mwa juma lililopita, FC Barcelona walifanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja, yaliyofungwa na Jeremy Mathieu pamoja na Luis Suarez.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment