Taasisi ya Ilawa Improvement ya Mkoani Njombe Yataka Lowassa Apitishwe Kugombea Urais.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeombwa kutumia busara wakati uteuzi wa jina la mgombea urais kwa kupitia chama hicho kuangalia mtu anayependwa na wananchi bila kukiathiri kwa kuteua mtu asiyekubalika.

Wamempendekeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (pichani), kuwa ndiye wanayemuona anaefaa kutokana na kukubalika.

Wito huo ulitolewa na taasisi ya Ilawa Improvement ya mkoani Njombe kupitia Mwenyekiti wake, Nathaniel Mgani, ambaye alisema vikao vya CCM vitakapompendekeza mtu atakayemrithi Rais Jakaya Kikwete iangalie mtu anayekubalika kwa watu ili kutopoteza mvuto wa chama kwa wananchi katika uchuguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

“Kwa niaba ya taasisi yetu tunapendekeza wanapoangalia mtu wa kumuweka kugombea urais wahakikishe wanaweka mtu anayekubalika kwa watu ili kuepuka anguko kubwa, sisi kama Ilawa tunampendekeza Edward Lowassa kuwa mgombe wa urais,” alisema Mgani.

Aidha, alisema wakati Lowassa akiwa waziri mkuu hapakutokea mauaji ya ovyo ya raia wala vurugu katika maeneo nchini.
Mgani alisema Lowassa alipokuwa waziri mkuu hata Rais Jakaya Kikwete hakupata shida kwa kuwa alikuwa na kiongozi aliyekuwa anaisimamia serikali yake na kuwa ilikuwa imetulia.

Aliongeza kuwa wanamuona Lowassa ni kiongozi bora kutokana na alivyosimamia maendeleo katika jimbo lake la Monduli ambalo lina barabara nzuri, huduma za afya na huduma zingine za kijamii zenye uhakika tofauti na maeneo mengine ya nchi.

Aliiomba Kamati Kuu ya CCM kumpitisha Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM kushindana na vyama vya upinzani kutokana na jina lake kuwa masikioni mwa watu wengi na kwa kufanya hivyo chama hicho kitapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment