Wabunge kwa kauli moja wametaka itungwe sheria ili kuweza kudhibiti wizi wa fedha za wananchi kupitia ATM na Miamala mbali mbali zinazofanywa kupitia simu za mkononi ambapo wamesema kuwa ikiwepo sheria itawapa unafuu watanzania wengi ambao wanaibiwa huku wakishindwa kujua ni nani atupiwe lawama.
Baadhi ya wabunge waliokuwa wanahimiza kutungwa kwa sheria hiyo wameyatupia lawama baadhi ya makampuni hayo ya simu kuwa yamekuwa yakiwaunganishia wateja kwa mambo mbalimbali kama nyimbo na promosheni nyinginezo bila idhini ya mtumiaji wa mtandao huo huku wakikata kiasi cha fedha ambacho kinaendana na promosheni zao ambazo mtumiaji anakuwa aelewi nini manufaa yake.

Kwa hili tunawapongeza wabunge wetu maana sisi watumiaji wa mitandao hii tulikuwa tunateseka sana kutokana na kukatwa kiasi cha fedha ambacho hatujui kinapelekwa wapi.
0 comments:
Post a Comment