Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ametembelea ofisi ya Chama hicho iliyoteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana kwenye jimbo la Dimani.
Mara baada ya ukaguzi huo Maalim Seif alisema kitendo hicho ni cha kulaaniwa na hakipaswi kufanyika katika kipindi kama hiki.
Alisema matendo ya namna hii yalikua yakifanyika katika zama za siasa za Chuki visiwani Zanzibar ambapo kwa sasa zimeondoshwa baada ya uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Aidha Maalim Seif ametoa wito kwa wanachama wa Chama cha CUF kutolipiza kisasi kwani kufanya hivyo kutasababisha uwepo wa uvunjanji wa Amani.
0 comments:
Post a Comment