Zitto Kabwe: Nipo Tayari Kufanyiwa Uchunguzi

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, ameombwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), zichunguzwe.
“Naiomba Sekretariati ya maadili iyachukue kwa uzito maoni ya Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu wa sheria na kanuni yafanyiwe uchunguzi. Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi,” amesema. 
Hatua hiyo inakuja baada ya Ngeleja kumtaja Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), kuwa amepokea mgawa wa fedha za kutoka akaunti ya Escrow sh. milioni 30 lakini Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma halijamwita kumhoji.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Zitto amesema katika kujitetea mbele ya Baraza la Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Escrow, Ngeleja amesema kuwa ni kawaida wabunge kupewa misaada na wafanyabiashara na taasisi za umma.
“Katika maelezo yake alirudia tuhuma za kipuuzi dhidi yangu zilizokwisha tolewa huko nyuma kwamba nilipewa fedha na kampuni ya PAP na nilipewa fedha na shirika la NSSF.
“Tuhuma zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo,” amesema Zitto.
Kwa mujibu wa Zitto, watuhumiwa wa ufisadi wa escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa na hivyo wanajaribu na watajaribu kubwabwaja na kuhangaika ikiwemo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao.
Zitto ameongeza kuwa ndio maana Ngeleja ametaja msururu wa watu wakiwemo wafanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila chembe ya ushahidi. 
“Hivyo, narudia kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja, wenye ushahidi wapeleke kwenye vyombo vya uchunguzi na niitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza.
“Nikiwa mbunge ambaye maisha yangu yote ya siasa nimeyatumia kupambana na ufisadi na kuchochea mabadiliko ili kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji na kuimarisha taasisi zake, nipo tayari kwa uchunguzi mahususi dhidi yangu dhidi ya tuhuma zilizotolewa na nyingine zozote ambazo mtanzania yeyote anazo dhidi yangu,” ametamba Zitto. 
Mbunge huyo ameungwa mkono kwa nguvu kubwa kazi inayofanywa na Baraza la Maadili. Kwamba ni kazi ambayo ilipaswa kuwa imefanyika kwa muda mrefu sana kwa kashfa mbali mbali ambazo viongozi wa umma wamepata kama vile ile ya rada, rushwa katika manunuzi ya mafuta mazito kuendesha mitambo ya umeme, kujipatia mikopo kwenye taasisi za umma bila kulipa, kujilimbikizia mali tofauti na kipato.
“Naiomba Sekretariati ya maadili iyachukue kwa uzito maoni ya Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu wa sheria na kanuni yafanyiwe uchunguzi. Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi,” amesema. 
Zitto ameongeza kuwa katika kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji nchini ni lazima kila kiongozi aheshimu taasisi kama Baraza la Maadili.
Amesema kuwa Baraza likiendelea kufanya kazi kama inavyofanyika sasa, vita dhidi ya ufisadi itakuwa imepiga hatua na porojo za kuzushiana mitaani zitapungua. 
Credit: Mwanahalisi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment