AZAM TV Yashinda tuzo ya Super Brands 2014/15

Washindi wa super brands 2014/15 kwa Upande wa Tanzania wametangazwa hii leo jijini DSM ambapo orodha hiyo inahusisha matokeo kwa kampuni zinazotoa huduma na kuzalisha bidhaa mbali mbali,
hata hivyo baada ya majumuisho ya utafiti na uchambuzi wa kina uliofanywa na idara ya uchambuzi wa viwango yenye makao makuu nchini Uingereza kwa kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko na maoni ya watumiaji zaidi ya 1000 wa huduma hizo.
Kwa mara ya kwanza kampuni ya Bakhresa Group imetoa washindi wawili Huku Azam ikishika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Bakhresa katika nafasi ya pili.
Hii ni mara ya kwanza kwa Azam kufika nafasi ya juu zaidi katika orodha ya super brands ikiwa imepanda nafasi 11 zaidi kufika kileleni, kutoka nafasi 12 ikilinganishwa na majumuisho ya 2013/ 14 huku Bakhresa wakiingia 20 bora.
Hii inamaanisha kwamba bidhaa zote zinazozalishwa na Azam pamoja na Bakhresa zimetwaa tuzo hizo za kimataifa duniani na kufanya kua makampuni bora 2014/15
Jumla ya kampuni 11 zinazotoa huduma na kuzalisha bidhaa zimeendelea kung’ang’ania kwenye orodha ya 20 bora ya super brands ikilinganishwa na majumuisho ya 2013/14.


ITV na Clouds Fm walionekana kuwa kampuni mbili bora 2013/ 14 wamebaki kwenye orodha ya 20 bora ingawa wameshuka kutoka nafasi zao msimu uliopita ITV wakiwa nafasi ya nne Clouds wakiwa nafasi ya nane.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment