Spika Makinda Akabidhi Miswada ya Habari Kamati ya Bunge

Wakati wadau wa habari wakimwomba Spika wa Bunge, Anne Makinda (pichani), atumie busara kuishauri serikali iwasilishe miswada miwili ya habari ya mwaka 2015, wa Haki ya Kupata Taarifa na ule wa Huduma za Vyombo vya Habari kwa kawaida, Spika Makinda amesema ombi hilo amelipeleka kwenye kamati husika ya Katiba, Sheria na Utawala.
Aidha, Spika Makinda amesema wadau wowote wenye maoni kuhusu miswada hiyo waiwasilishwe kwenye Kamati hiyo ya Bunge.
Spika Makinda aliyasema hayo kwenye viwanja vya Bunge mjini hapa baada ya NIPASHE kutaka kujua kama mapendekezo hayo ya wadau yanaweza kusikilizwa.
Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge, miswada hiyo itawasilishwa Jumanne ijayo chini ya hati ya dharura.
Kwa mujibu wa maombi hayo, wadau hao ambao wamejichimbia Dodoma tangu Jumamosi iliyopita wamemuomba Spika kutumia madaraka yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi kuishauri serikali kuwasilisha miswada hiyo katika utaratibu wa kawaida ili kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kabla ya kupitishwa kuwa sheria.
Barua pia imeandikwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ikimuomba naye aone umuhimu wa wananchi kushiriki kutoa maoni katika miswada hiyo kabla ya kupitishwa na Bunge kwenye mkutano wa 19 unaoendelea mjini Dodoma.
Naye Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ameandikiwa barua na wadau hao wakimuomba atumie nafasi yake kama msemaji mkuu wa kambi hiyo bungeni kuishauri serikali iwasilishe miswada hiyo chini ya mfumo wa kawaida na siyo chini ya hati ya dharura kwani unawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni yao kwenye miswada hiyo kabla ya kupitishwa na Bunge.
Tangu serikali iseme kuwa inakusudia kuwasilisha miswada hiyo chini ya hati ya dharura, wadau wa habari wamekuwa wakiomba ibadili msimamo kwani kufanya hivyo kutawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni juu ya miswada hiyo kabla ya kuwa sheria.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, kwa niaba ya Mbowe, amesema amepokea barua ya wadau.
Alisema jana kuwa kwa niaba ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, ametambua na kukubali ombi hilo na Kambi Rasmi ya Upinzani itatoa ushauri huo kwa Serikali na kusimamia utekelezaji wake.
Chanzo: NIPASHE
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment