Mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus FC wamefuzu kwa hatua ya robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Borussia Dormund usiku huu Uwanja wa Westfalenstadion, Dortmund, Ujerumani.
Juventus wamefuzu kwa hatua hiyo kwa jumla ya ya mabao 5-1, baada ya awali kupata ushindi mwembamba katika uwanja wao wa nyumbani wa 2-1.
Juventus wamefuzu kwa hatua hiyo kwa jumla ya ya mabao 5-1, baada ya awali kupata ushindi mwembamba katika uwanja wao wa nyumbani wa 2-1.
Aliyekua mshambuliaji wa Man City na Man Utd Carlos Tevez aliifungia Juve bao la kwanza dakika ya tatu, kabla ya Alvaro Morata kufunga la pili dakika ya 70 baada ya kupokea pasi kutoka kwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Argentina.
Tevez aliongeza bao la tatu na la ushindi zikiwa zimesalia dakika 10 na hicho kinakuwa kipigo cha nne kwa Dortmund katika michezo minne waliyokutana na Juventus kwenye michuano ya Barani Ulaya.
Timu nyingine zilizotinga Robo Fainali ni PSG, Monaco zote za Ufaransa, Atletico Madrid, Real Madrid, Barcelona, FC Porto na Bayern Munich.
Droo ya Robo Fainali itapangwa Ijumaa Saa 7:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment