Nick wa Pili Awafungukia BASATA Juu ya Uboreshaji wa Tuzo za KTMA Msimu wa Mwaka Huu

Wiki iliyopita ilifanyika tathmini ya tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) za mwaka jana, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye msimu mpya wa tuzo hizo kwa mwaka huu 2015.

Kwa kawaida Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) hualika wadau mbalimbali kuhudhuria tathmini ya tuzo za mwaka uliopita kwa lengo la kuwapa nafasi ya kutoa maoni ya maboresho kabla ya msimu mpya kuanza. 

Joh Makini na G-Nako wa Weusi ni miongoni mwa wasanii walioalikwa na kuhudhuria kikao hicho cha tathmini, na baada ya kujikuta ni wao pekee ndio wasanii waliohudhuria kati ya wasanii wote waliopewa mualiko, Nikk Wa Pili alikuwa na haya ya kusema: 

“TUZO ZINAKUWAGA NA MALALAMIKO MENGI..LEO BASATA WALI ALIKA WASANII KUJA KUTOWA MAONI YAO KUBORESHA TUZO. KATIKA WASANII WALIO ALIKWA NI WASANII WAWILI TUUU WALIOFIKA AMBAO NI G.NAKO NA JOH MAKINI…KIKAO KILI UDHURIWA NA BRAND MANAGER WA KILIMANJARO NA WATU WA BASATA……HAYA TUSUBIRI TUZO ZIJE TUMWAGIKE MITANDAONI KWA LAWAMA” Nikk aliandika kupitia Instagram.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment