Chadema Yanasa Taarifa za Siri za Kumuua Dk. Slaa Hizi Hapa Zisome Ujue nawe

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Madendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema kwamba kuna mawasiliano ya siri yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya chama hicho, na mkakati wa kumdhuru Katibu Mkuu, Dk Willibroad Slaa.
Amesema kuwa Idara ya Usalama wa Taifa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula, wamekuwa wakimtumia Khalid Kagenzi-mlinzi binafsi wa Dk. Slaa ili kurekodi na kuvujisha taarifa za vikao vya siri vya Chadema.
“Kama chama tumelalamikia sana serikali ya CCM kwa matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi yetu. Sasa tumebaini wanatumia vijana wetu kunasa taarifa zetu.
“Kagenzi kwa miaka miwili tumebaini amekuwa akitumika kupeleka taarifa za Chadema kwa usalama wa taifa. Amekiri hilo kwa maandishi na kutaja namba za watu wa usalama anaowasiliana nao,” amesema.
Marado alimtuhumu Mangula kuwa imebainika anawasiliana na Kagenzi ikiwa ni pamoja na kumtumia fedha mara mbili, Julai 24 na Desemba 4 mwaka jana, kupitia simu yake ya Vodacom (anaitaja).
Kwa mujibu wa Marandu, mlinzi huyo alipobanwa zaidi alieleza mkakati uliokuwa ukipangwa na watu hao wa kumwekea Dk. Slaa sumu kwenye chakula au kinywaji.
Amesema kuwa wamebaini nyendo hizo hivi karibuni baada ya mlinzi huyo kuonekana akipanda katika gari ya afisa usalama wa mkoa wa Kinondoni lenye namba za usajili T213 ARS, akiwa nalo afisa msaidizi.
Marando amefafanua kuwa watamfikisha Kagenzi polisi ili achunguzwe na hatua zaidi zichukulie, lakini akakataa kuweka hadharani namba za simu na majina ya maafisa usalama aliodai wako zaidi ya 22.
Amesema kuwa pia wamenasa taarifa za maofisa hao za kumtumia Kagenzi muda wa maongezi zaidi ya shilinigi milioni saba kwa nyakati tofauti.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment