Fareed Kubanda amepewa heshima kubwa na EU. Rapper huyo jana alitunikiwa tuzo iitwayo ‘Champion of the 2015 European year for development in Tanzania’ kutoka kwa umoja wa nchi za Ulaya kutokana na mchango wake katika jamii kupitia mambo tofauti anayoyafanya kupitia muziki wake.
Fid amesema kuwa tuzo hiyo ni kama endorsement ambayo ameahidiwa na umoja huo huo kufanya naye kazi mbalimbali. “Hakuna kitu kizuri kama kufanya kitu sahihi na kizuri halafu watu wakakiona na kuonyesha kukipokea na kukikubali,” amesema Fid.
“Kwa sababu kuna wasanii wengi wanafanya vitu vizuri, vitu vyenye umuhimu katika jamii, lakini kwa namna moja au nyingine hawapati bahati ya shughuli zao zile kufikia masikio ya wengi.
Kwahiyo hii kwangu mimi ni kama bahati kwa sababu kulikuwa kuna wasanii wengi Licha ya kupewa cheti cha heshima hiyo, hii ni kama endorsement itakayoniwezesha kufanya nao kazi mbalimKuna watu walikuwa wanafuatilia muziki wangu tangu zamani, wameangalia nafanya nini kwenye nyimbo zangu, nimekuwa nikijihusisha na kazi mbalimbali za jamii.
Nimekuwa mstari wa mbele kuzungumzia na kuanzisha project mbalimbali kuhusu kupambana na HIV, HIP HOP Darasa na mengine. Kwahiyo hayo yote wakaona kuwa mimi ndio nafaa kupewa heshima hiyo.
Hii ni kama changamoto kwa wasanii wengine kujaribu kuwa mfano bora kwa jamii kupitia mambo tunayoyafanya, kwa sababu sisi tumepewa nguvu za kuzungumza na kueleweka na jamii.”
0 comments:
Post a Comment