Profesa Lipumba : Sigombei Ubunge Temeke Wala Tabora

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema hana mpango wa kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.
Vilevile Profesa Lipumba ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, hakukubali wala kukataa alipoulizwa iwapo atajitosa kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya umoja kwa nafasi ya urais.
“Mimi naulizwa na ninasikia wanasema nitagombea Temeke au Tabora Kaskazini. Mimi sina utaratibu wala sijaota na sina mpango wowote wa kugombea ubunge,” alisema alipotembelea ofisi za gazeti hili, Tabata Relini Dar es Salaam jana.
Profesa Lipumba akijibu swali kama hakuwa na mpango wa kugombea ubunge, je, ana mpango wa kugombea urais kupitia Ukawa, alijibu; “Sasa nani atakuwa mgombea hilo ni jambo ambalo (Ukawa) hatujalifanyia uamuzi, bado lipo katika utaratibu,” alisema na kuongeza;
“Siwezi kusema kwamba nitagombea nafasi ya urais kwa sasa, mgombea ndani ya umoja wetu bado hajapatikana kama atatoka nje ya CUF mimi nitamuunga mkono atakayependekezwa.”
Tangu Novemba mwaka jana vyama vya CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na NLD vimekuwa katika majadiliano ya kuachiana nafasi katika majimbo ya uchaguzi kwa nafasi za ubunge na udiwani ili viweze kusimamisha mgombea mmoja kila sehemu lengo ni kuishinda CCM.
Lipumba amegombea urais mara nne, akiwa ameshika nafasi ya pili mwaka 2000 na 2005 na mwaka 2010 kushuka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Dk Slaa na Rais Jakaya Kikwete.
Profesa Lipumba akizungumzia suala Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na iwapo kuna mazungumza ya kujiunga CUF, alisema suala hilo ni nyeti hasa ukizingatia na mazingira yake yaliyopo ya sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
“Sijapata fursa ya kuzungumza naye (Zitto) lakini sina taarifa yeyote kama anakuja CUF au nini kwani uanachama ni suala linalofanyika ngazi ya tawi siyo huku Taifa.”
“Zitto ana akili sana, anajua kuchambua na kujenga hoja lakini naheshimu kwa wenzetu wa Chadema kwa muda mrefu wamekuwa na hoja nzito kuhusu yeye. Kwa kuwa hawa tuna ushirikiano, basi hatuna budi kukubaliana nao.
Credit: Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment