Balozi wa kujitolea wa Harakati za ‘Imetosha Movement’, Henry Mdimu, amekanusha uvumi ulioenea hasa katika nchi za nje, unaodai kwamba serikali imekataza watu wenye ulemavu wa ngozi kuandaa matembezi au maandamano na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Mdimu amesema baada ya taratibu kukamilika, matembezi ya hisani yatafanyika Machi 28 mwaka huu kuanzia saa 12 alfajiri, katika viwanja vya Leaders Club, ambapo watazunguka katika maeneo yaliyoorodheshwa na kurudi katika viwanja hivyo.
Amesema kuwa matembezi hayo yatakuwa kwa ajili ya kuchangia fedha zitakazowezesha kutolewa kwa elimu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa juu ya imani potofu zinazoendelea na mauaji ya albino yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Machi 28, 2015.
Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni kujitokeza katika matembezi hayo ya hisani ili kuunga mkono juhudi za mapambano ya kukomesha mauaji na vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino maeneo mbalimbali ya nchi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment