Zitto Kabwe Kuaga Wabunge Wenzake Leo

Dodoma, Tanzania. Taarifa kutoka katika magazeti ya Nipashe na Mtanzania zinaeleza kwamba Mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe anapanga kuaga wabunge wenzake leo.

Mbali na hayo taarifa zinaeleza kuwa Zitto Kabwe alitaka kuaga jana kabla ya kukabidhiwa barua na chama chake, lakini alitulizwa na Spika Anna Makinda.

Zitto alishindwa kufanya hivyo baada ya kuitwa na Spika Makinda kwa ajili ya mazungumzo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja  vya Bunge jana, Zitto alisema: “Hizo tetesi zipo tu, ukifika muda mtajua kila kitu.

“Sasa hivi naenda kuzungumza na Spika, ameniita, nitakuwa na mazungumzo naye.”
Zitto alisema tetesi za kuwaaga wabunge zitathibitika muda utakapofika.
Katika gazeti la Nipashe linaeleza kwamba siku 8 zamsubiri Zitto kujiunga rasmi na chama cha ACT.

Chanzo:Nipashe/Mtanzania.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment