Baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zamani Mark Lippert akimuombea apone haraka baada ya kutokea kwa shambulio hilo.
Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji kwa zaidi ya saa mbili. Madaktari wamesema kuwa majeraha yake hayatarishi maisha yake.
Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta 11 na ameshonwa nyuzi 80 kwenye mkono uliochomwa kwa kisu na kusababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote .
0 comments:
Post a Comment