Msanii Jaguar Akili AY Kumtoa Kimuziki

Msanii Jaguar kutoka Kenya ambae kwa sasa anafanya poa na ngoma yake ya 'HUU MWAKA' amefunguka na kusema kuwa msanii kutoka Tanzania Abwene Yesaya alikubaliana nae kufanya collabo.


ili hali wakati huo hakukuwa na mtu yoyote anaemjua katika tasnia ya muziki,Jaguar amefunguka hayo leo kupitia ukurasa wake wa Instgram
Jaguar amekili wazi kuwa Msanii Ay ndie aliemtambulisha katika ulimwengu wa muziki kwa kukubali kufanya nae kazi yake ya kwanza ambayo ilifahamika kama Nimetoka mbali
na video yake kufanywa na Ogopa Video ambayo ilitoka mwaka 2009 Agust.
Katika wimbo huo ambao uliweza kupokelewa vizuri na mashabiki kwa kipindi hicho ulikuwa ukielezea namna wasanii hao wanaweza kuvuka mipaka na kufika mbali katika
muziki wao ambapo hilo limejidhirisha wazi kwa wasanii hao kujitahidi kufungua mipaka ya muziki wao ukifananisha na wasanii wengine ndani ya nchi yao kila mmoja mmoja.
"Will always be grateful to this guy AY for accepting do a collabo with me when nobody knew me....Tuzidi kuvuka boda"
Msanii AY ni moja kati ya wasanii na wapambanaji katika tasnia ya bongo fleva ambae alitumia nguvu yake kubwa kutanua muziki wa Afrika Mashariki na baadae aliweza kuwa
msanii wa kwanza kufanya kazi na wasanii mapacha kutoka nchin Nigeria P Square na J Martin,lakini pia aliweza kuvuka boda zaidi na kuweza kufanya kazi na wasanii kama
La'myia, Ms Triniti pamoja na Sean Kingstone katika kazi mbalimbali ambazo zimezidi kumuweka AY katika nafasi nzuri kimuziki kimataifa.
Lakini kwa upande wa Jaquar baada ya kazi yake ya kwanza kumtambulisha vizuri aliendelea kutoa kazi mbalimbali ambazo alikuwa akifanya single lakini mwaka jana aliweza
kuachia kazi yake ya msanii kutoka Nigeria iliyofahamika kama One Centimeter.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment