Mshambuliaji kutoka nchini Togo, Emmanuel Sheyi Adebayor ametuma salamu kwa wapinzani wa klabu ya Tottenham Hotspurs, kwa kusema yupo tayari kuisaidia klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London kufuatia matatizo yaliyokua yakimsumbua kumalizika.
Adebayor mwenye umri wa miaka 31, alirejea uwanjani mwishoni mwa juma lililopita kuitumikia Spurs, wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Man Utd.
Adebayor amesema baada ya kukamilisha kila jambo ambalo lilikua likimsibu na kushindwa kujumuishwa uwanjani kisawa sawa, atafanya jitihada ili kurejesha hali yake ya awali alipokuwa akicheka na wavu na kuwatesa walinzi wa safu za timu upinzani.
''Kwa hakika mambo mengi tu yamefanyika maishani mwangu mambo ambayo yameniathiri kwa kiasi kikubwa lakini sasa hali imerejea kuwa shwari namshukuru mola''
''Sote ni binadamu, leo utafaulu kufanya jambo kesho itakuwa zamu ya mwengine lakini kwa wakati uliopita maisha yalinipiga chenga, na nikayaruhusu kuingilia mchezo wangu na umakini wangu''
''Sasa nimerejea uwanjani mzima, mzima.''
''Mimi si kijana mwenye umri wa miaka 21 la hasha, mimi sasa nimegonga miaka 31 na hivyo napaswa kuonesha ukomavu wangu uwanjani''
''Tumesalia na michezo tisa ya ligi kuu na hilo linamaanisha nitakuwa hapa kwa zaidi ya miezi miwili, chochote chaweza kutokea. Alisema mchezaji huyo
Adebayor alipoteza makali yake katika hali ya mshtuko mwanzoni mwa msimu huu, na kufikia hatua ya kuwakera mashabiki wa Spurs ambao walimtarajia kwa mengi, baada ya kufanya vyema mwishoni mwa msimu uliopita.
Mpaka sasa Adebayor ameshaifungia Spurs mabao mawili katika michezo kumi na sita aliyochezwa kwa msimu huu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment