Chama kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT) kimetangaza kuitisha mkutano mkuu wa taifa Machi 28, 2015.
ACT kimetangaza mkutano huo kupitia tangazo lake na kwamba mkutano utahusisha wanachama wake tu.
Mbali na na mkutano huo pia chama hicho kitazinduliwa rasmi Machi 29, 2015 na kuwaomba watu kuhudhuria katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Chama cha ACT kilianzishwa na Samson Mwigamba (anayedaiwa kuwa mfuasi wa mbunge Zitto Kabwe) na kupewa usajili wa muda huku kikitamba kuwa mbadala wa vyama vyote vilivyopo sasa kwa maelezo ya kuwa vimekosa demokrasia ya kweli.
Mwigamba aliwahi kuwa mmoja wa viongozi wa Chadema ambaye alikuja kuvuliwa uanachama wake na kuamua kuibukia ACT.
Hata hivyo kuna taarifa cha chini kwamba mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambaye amevuliwa uanachama wake Chadema mapema wiki hii anaweza kuhamia chama hicho na kuweza kukiongoza.
0 comments:
Post a Comment