Mayanja: Andrew Shamba Aliwabeba Yanga Kwa Makusudi

Kocha mkuu wa Kagera Sukari, Jackson Mayanga amemtupia lawama muamuzi Andrew Shamba kwa kumtaja kuwa chanzo cha kupoteza mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara hapo jana.

Mayanja raia wa nchini Uganda alisema muamuzi huyo aliwaathirti kwa kiasi kikubwa wachezaji wake kutokana na maamuzi ambayo yaliiwezesha Dar es salaam Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Kocha huyo alidia kwamba endapo soka la Tanzania litaendelea kwa lengo la kuibeba timu moja ama nyingine kwa maslahi ya wachache bado kuna kazi kubwa ya kufanya, hasa ikizingatiwa waliokua wakicheza nao ni wawakilishi pekee wa michuano ya kimataifa.

“Kila siku nikija hapa huwa ninawaambia nyingi waandishi hamuweki mambo hadharani watu wakajua, suala ni kwamba waamuzi wamekua wakiua soka la nchi hii kutokana na matatizo ya kushindwa kutoa haki uwanjani”

“Lengo ni soka lichezwe kwa haki ili kila mmoja aondoke uwanjani akiwa ameridhika na matokeo, lakini kwa leo ninarejea tena muamuzi hakututendea haki na hii sio mara moja, kwani tumekua tukisema kila siku waamuzi wanaziumiza timu nyingine hasa zinapokutana na timu zinazoitwa timu kubwa.” Alisema Mayanja

Wakati Mayanja akimtupia lawama muamuzi Andrew Shamba, kocha wa Dar es salaam Young Africans, Hans van Pluijm aliwaponda wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango kibovu katika mchezo wa jana licha ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Alisema kulikua na tofauti kubwa na mchezo waliocheza mwishoni mwa juma lililopita na kufanikisha ushindi wa mabao matano kwa moja dhidi ya FC Platnum.

“Hatukucheza vizuri, hakukua na pasi za uhakika kama zilizoonekana wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma na sikufurahishwa na hilo, japo nawapongeza wachezaji wangu kwa kuzipata point tatu dhidi ya Kagera Sukari”

Ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Kagera Sukari umeirejesha Dar es salaam Young Africans kileleni kwa kufikisha point 34 na kuishusha Azam FC ambao walipanda kileleni kwa kufikisha point 32 baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Ndanda FC uliochezwa siku ya jumatatu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment