Mhe: Samuel Sitta Kukaimu Nafasi ya Waziri Mkuu Katika Bunge la 19.

Kikao cha Kumi na Tisa cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimeanza rasmi hivi leo mjini Dodoma na Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta ameachiwa nafasi ya kukaimu nafasi ya Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda katika msimu huu wa bunge kutokana yeye kuwepo safarini nchini Japan kikazi ambapo amekwenda kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe.Dkt Jakaya Kikwete.

Katika kipindi cha maswali na majibu Mhe Josephine Genzabuke Mbunge wa Viti Maalum aliuliza swali kuhusu kuwepo na watu wanaoshukiwa kuwa ni wakimbizi katika Mkoa wa Kigoma waliyopiga kura katika kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Disemba mwaka jana.

Naye Waziri wa Tamisemi Mhe.Aggrey Mwanri akijibu swali hilo kwa kusema kuwa serikali itafuatilia swala hilo kwa kushirikiana na Mbunge wa Kigoma ilikuchunguza suala hilo pamoja na kuchukua hatua za haraka katika kulipatia ufumbuzi.

“Ni jukumu la viongozi wa vijiji,vitongoji na mitaa pamoja na wananchi kuwabaini watu ambao siyo raia au wakazi wa eneo husika na kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua ziweze kukuchukuliwa kwa mujibu wa sheria”alisema Mhe.Mwanri.

Mhe.Mwanri aliendelea kusema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulifanyika kwa kuzingatia kanuni za uchaguzi kwa kuangalia vigezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuangalia vigezo kama kila mpiga kura ni lazima awe raia wa Tanzania, awe na umri wa miaka kumi na nane au zaidi, awe mkazi wa eneo hilo,pia wapiga kura wote walitakiwa kujiandikisha na kwa maeneo waliyo gunduwa kuwepo na watu wasio raia wa kitanzania na walitaka kupiga kura waliwekewa pingamizi.

Kwa upande wa maswala ya Afya Mhe.Moza Saidy Mbunge wa Viti Maalum aliuliza swali juu ya chanjo zinazotolewa kwa watoto na watu wazima ikiwa chanjo hizo zinatoka nje ya nchi kama msaada zinahakikiwa katika maabara zipi nchini kuona ubora wake.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe.Dkt Steven Kebwe alisema serikali inasisitiza kuwa chanjo zote zinazotolewa katika vituo vya afya nchini na mashuleni ni salama na jamii huelimishwa kuhusu chanjo kwa kutoa elimu kupitia vyombo vya habari kama radio,runinga,magazeti,mabango na vipeperushi.

“Uhakiki wa Ubora na Usalama wa chanjo hizo hufanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa katika maabara yake na hufanya ukaguzi wa chanjo zote zinazoingia nchini kwa lengo la kudhibiti ubora na usalama pamoja na kuhakikisha chanjo hizo zimeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani”,alisema Mhe.Dkt Kebwe.

Hivyo kutokana na kutolewa kwa elimu kuhusu manufaa ya chanjo mwitikio umekuwa mkubwa sasa na kufikia kiwango cha asilimia 90 kwa mwaka 2012-2014 sawa na malengo ya kitaifa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment