Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania imesisitiza kuwa mvua kubwa zaidi ambazo ni milimita 50 zilizonyesha sasa zitaendelea kunyesha jijini Dar es salaam hadi machi 25 mwaka huu.
Akizungumzia utabiri huo Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hai ya hewa Dk. Agnes Kijazi amesema kwamba mvua kubwa za milimita 50 zitaendelea kunyesha kwa siku tatu mfululizo.
Siku tatu mfululizo mvua kubwa imenyesha katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu watano huku nyumba kadhaa zikiathirika kutokana na mvua hizo hasa katika maeneo ya Jangwani, Bonde la Mto msimbazi pamoja na msasani.
Mamlaka ya hali ya hewa imewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya utabiri huo ili kujiepusha na madhara yanaweza kutokea.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment