Garcia: Wakinitaka Niende, Nitakwenda

Meneja wa klabu ya AS Roma, Rudi Garcia amesisitiza kuwa tayari kujiuzulu nafasi yake klabuni hapo endapo atashinikizwa na uongozi kufanya hivyo kutokana na hali halisi iliopo huko Stadio Olympico mjini Roma.

AS Roma, wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya nchini Italia Serie A, na wamekua hawafanyi vizuri tangu mwishoni mwa mwaka jana ambapo tangu sikuku za Christmas na mwaka mpya wameshinda mchezo mmoja kati ya michezo kumi hali ambayo imepelekea kupoteza point 14.

Mustakabali wa Garcia klabuni hapo umekua ukitajwa kuwa mashakani kutokana na hali inayomuandama, na tayari aliyekua meneja wa klabu za SSC Napoli pamoja na Inter Milan, Walter Mazzarri anatajwa kuchukua nafasi yake kuanzia msimu ujao wa ligi.

"Siku niliyokubali kuichukua AS Roma, sikuahidi kama nitaiwezesha kutwaa mataji kila kukicha hivyo linalotokea sasa ni hali ya mchezo wa soka ambao una matokeo ya kustaajabisha kutokana na vipindi tofauti," Alisema Garcia

"Lakini ninaamini wachezaji wapo pamoja nami, na hawafanyi makusudi kupata matokeo mabovu kama wengi wanavyodhani, zaidi ya kila mmoja wetu kuwa na matumaini ya kutaka kushinda kila mchezo na ndio maana kila siku nipo hapa tukisaidiana na wengine.

"Ninasema sitokuwa king’ang’anizi endapo uongozi utaonyesha kutokua tayari kunipa ushirikiano katika kipindi hiki kigumu na hatimae kunitaka niondoke ili mwingine achukue nafasi yangu klabuni hapa." Aliongeza Garcia

Katika hatua nyingine meneja huyo kutoka nchini Ufaransa amesisitiza suala la kikosi chake kuwa katika hali ya utayari kwa lengo la kupambana na Fiorentina katika mchezo wa mkondo wa pili wa Europa League, baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kushuhudia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Amesema kikosi chake kina matarajio ya kushinda mchezo huo, laini anaamini hata wapinzani wao wana malengo kama hayo, hivyo atakipeleka kikosi chake uwanjani kupambana kwa lengo la kuhitaji kusonga mbele, japo lolote laweza kutokea.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment