Sakata La Zitto Kabwe Lasukumwa Kwa Spika

Hatma ya ubunge wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuendelea au kutoendelea kuwa Mbunge imebainika kuwa Spika wa Bunge Anne Makinda ndiye mwamuzi wa mwisho katika Suala hilo.

Aidha,Mwanasiasa huyo machachari ndani na nje ya nchi hivi karibuni ametangaza rasmi kutogombea tena katika jimbo lake la kigoma Kaskazini jambo lingine linalowaweka washangazwa maelfu ya wananchi pamoja na wafuasi wake nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akizungumzia suala la zito kuvuliwa uanachama amesema kwamba suala la Mbunge Zitto Kabwe kusimamishwa bado halijawafikia rasmi ikihusisha taarifa ya Mahakama kuhusu kufutwa kwa kesi yake.

“Kitu chenyewe kinachotokea ni kuarifu Tume ya Uchaguzi kwamba huyu mtu sasa hayupo.. Suala lenyewe lilikuwa Mahakamani, sisi lazima tupewe official communication“– Alisema Spika Anne Makinda.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment