Dar es Salaam, Tanzania. Serikali ya Tanzania imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia juzi Machi 3 hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, uamuzi huo ulitangazwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia mbele ya viongozi wa TFF na benki ya CRDB iliyoshinda tenda ya tiketi hizo miaka mitatu iliyopita.
Hata hivyo, uamuzi wa kusitisha matumizi ya tiketi hizo umetolewa ikiwa ni siku nne kabla ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili.
Klabu hizo mbili zimekuwa zikipinga tiketi za kielektroniki tangu zilipoanza kutumika msimu uliopita pasi na kujali upotevu wa mamilioni ya shilingi kutokana na kutumika kwa tiketi feki katika mfumo wa kizamani zinaoung'ang'ania wa tiketi za kawaida.
0 comments:
Post a Comment